Wednesday, June 18, 2014

SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS KIKWETE

Uongozi  na Timu yote ya Tazama Ramani Tanzania inayosimamiwa, kuendeshwa na Kuratibiwa na  Chuo cha Utalii Udzungwa cha Mjini Moshi, Mkoani  Kilimanjaro tunapenda  kuchukua  nafasi  hii  kumpongeza  kwa  heshima  na  taadhima Rais  wa
Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Docta  Jakaya  Mrisho Kikwete  kwa  kutunukiwa  tuzo   ya Utumishi  Bora  kwa  kuwa  kiongozi   mwenye  mchango  mkubwa  zaidi  katika maendeleo  ya  Bara la Afrika  kwa  mwaka 2013. Tanzania na Watanzania  hii ni heshima kubwa  sana   na  tunu kwa Taifa letu  kwa  ujumla wake  kwa  kuthaminiwa  na  kutambuliwa  kwa kiongozi  wetu  katika   ugawa  Kimataifa.  Timu  yote  ni  uongozi wa Tazama   Ramani   Tanzania  tunakutakia  heri na fanaka,  nguvu na  hekima  zaidi  katika  utekelezaji wa  majukumu  yako  kitaifa  na  kizalendo. 

“ Tuwaelimishe,  Tuwahamasishe , Tuwathamini na  kuwawezesha  Watanzania  Wazalendo watalii wa ndani  nchini Tanzania katika  kuvitembelea  na  kuvifurahia vivutio vyao  asilia  vya  utalii  walivyobarikiwa na Mwenyezi  Mungu”
Edgardo K. Welelo. (Naipenda   Tanzania  na Watanzania).


Imetengenezwa na Fortune Media Work | Team Fortune